Arsenal na Liverpool wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Wolves na Algeria Rayan Ait-Nouri mwenye umri wa miaka 22 . (Football Transfers)
Liverpool wanataka kusalia na kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amevivutia na Flamengo ya Brazil na Al-Ettifaq ya Saudi Pro League. (Teamtalk)
Newcastle wanaenda kukagua mipango yao ya uhamisho wa Januari katika mkutano maalum wiki hii kufuatia jeraha la kiungo wa kati wa Brazil Joelinton, 27. (Guardian)
Chelsea hawana nia ya kumnunua mshambuliaji wa Sporting CP na Uswidi Viktor Gyokeres licha ya ripoti za ofa ya pauni milioni 73 kuwekwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.(Football London)
Brentford wamefanya makubaliano ya mdomo na Tottenham kwa ajili ya kumnunua kwa mkopo beki wa kushoto wa Uhispania Sergio Reguilon, 27, ingawa hakuna kipengele cha chaguo la kununua kwa mkataba wa kudumu (Fabrizio Romano kupitia X)
Paris St-Germain imeripotiwa kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kandarasi mpya yenye thamani ya euro 100m (£86.15m) kwa msimu ili kujaribu kusalia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (AS kupitia Mirror)
Manchester United wanamlenga mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 22, msimu wa joto. (Florian Plettenberg kupitia X)
Wolves wanafikiria kumnunua fowadi wa Albania Armando Broja, 22, ambaye mustakabali wake unaweza kutegemea iwapo Chelsea itasajili mshambuliaji mwezi huu. (Guardian)
Jose Mourinho anaweza kurejea katika usimamizi na klabu yake ya zamani ya Porto baada ya kutimuliwa na Roma siku ya Jumanne. (Express)
Arsenal wako kwenye mazungumzo na Besiktas kuhusu dili la kumnunua mlinzi wa Ureno Cedric Soares, 32 (Mail)
Mshambuliaji wa Burkina Faso Bertrand Traore na mlinzi wa Uingereza Calum Chambers, wote 28, wanavutia vilabu vya Uropa, baada ya kuambiwa wanaweza kuondoka Aston Villa mnamo Januari. (Football Insider)
BBC



