Simba - Local

BMT yaridhia rasimu ya Katiba Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Jan 2024
BMT yaridhia rasimu ya Katiba Simba

Baada ya mvutano wa miaka kadhaa hatimaye Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeridhia rasimu ya Katiba ya klabu ya Simba ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukamilika kwa mchakato wa Mabadiliko uliochukua takribani miaka mitano

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mwenyekiti wa kamati ya Katiba na Sheria wa Simba, Hussein Kitta amesema kamati yake imepokea barua kutoka BMT ikieleza kuridhishwa na yale yaliyopitishwa katika rasimu ya Katiba baada ya kufanyiwa marekebisho

Kitta amesema hayo yamefikiwa baada ya jitihada za pamoja kati ya Wizara yenye dhamana ya Michezo na Klabu ya Simba

"Waziri mwenye dhamana ya michezo aliitisha kikao kujadili kuhusu mchakato wa mabadiliko wa Simba na kukawa na mambo sita ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi"

"Kutokana na mkutano huo, bodi ya Simba ikaunda kamati hii. Tulipokea maoni mengi, mengine kwa barua pepe, mengine kwa barua, wengine kutupigia simu na kutumia ujumbe. Tulikaa vikao vinne kwa kati ya masaa 4-9"

"Lengo ni kukamilisha mabadiliko na serikali ilitupa muda ili kukamilisha jambo hili. BMT walisema kabla ya kupeleka kwa wanachama mlete hiyo rasimu tupitie kwanza. Baada ya vikao tukaenda BMT na nina furaha kuwambia kwamba tumepokea barua kutoka kwao ya kuridhishwa na yale tuliyopitisha"

"Mambo sita yaliyopitishwa yana faida zaidi kwa mwanachama wa Simba kuliko kwa mtu mwingine yoyote," alisema Kitta

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
29m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’