Atletico Madrid na Barcelona ni miongoni mwa takriban klabu sita zinazowania kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips kutoka Manchester City, huku mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ukitarajiwa kuamuliwa wiki ijayo. (Telegraph - usajili unahitajika)
Tottenham haijakata tamaa ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 23, kutoka Chelsea. (Football Insider)
Chelsea wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 22, kuondoka kwa mkataba wa kudumu iwapo ofa inayofaa itapokelewa, huku West Ham, Fulham na Wolves wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyowania. (Usajili unahitajika)
Mustakabali wa mshambuliaji wa Ureno Goncalo Ramos katika klabu ya Paris St-Germain uko mashakani na klabu hiyo ya Ufaransa inaweza kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari iwapo ofa inayofaa itatolewa. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Fulham wako kwenye mazungumzo ya kumsaini beki wa kati wa Chelsea Mwingereza Trevoh Chalobah, 24, kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita na chaguo la kumnunua. (Florian Plettenberg kwa Sky Germany)
Napoli itavutiwa na kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg ikiwa Tottenham itaamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mwezi Januari. (Telegraph - usajili unahitajika)
Arsenal wanaongoza kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons, 20, ambaye yuko kwa mkopo RB Leipzig kutoka Paris St-Germain. (Sport Bild kupitia Football Transfers)
The Gunners pia wamepewa nguvu katika kumsaka kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, kufuatia ripoti kwamba Newcastle inatafuta mbadala wake.(Football London)
Aston Villa wameulizia Borussia Dortmund kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Marekani Giovanni Reyna, 21(Football Transfers)
Marseille wanapanga kurejea kutoa ofa kwa winga wa West Ham Said Benrahma baada ya ofa ya kwanza kwa mchezaji huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka 28 kukataliwa.(Foot Mercato -Kwa Kifaransa)
Beki wa Romania Radu Dragusin, 21, anasema alikataa kuhama kwa dakika za lala salama kutoka Bayern Munich na kujiunga na Tottenham huku Spurs "wakinitaka tangu zamani". (Evening Standard)
Inter Milan wanakaribia kupata mkataba na mshambuliaji wa Iran Mehdi Taremi, 31, kuhamia klabu hiyo kwa uhamisho wa bure msimu wa joto baada ya mkataba wake na Porto kukamilika. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Beki wa Tottenham Muingereza Japhet Tanganga, 24, anatazamiwa kumaliza muda wake wa mkopo katika klabu ya Augsburg ya Ujerumani na kuhamia Millwall inayoshiriki Championship hadi mwisho wa msimu. (Evening Standard)
BBC