Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imerejea nchini wakitoka Ivory Coast kushiriki michuano ya Afcon 2023
Stars iliyokuwa kundi F, ilimaliza safari yake katika michuano hiyo ikishika nafasi ya nne ikikusanya alama 2 sawa na Zambia lakini timu hizo zikitofautiana mabao ya kufungwa
Katika kundi hilo DR Congo ilifuzu hatua ya 16 ikiwa na alama tatu na jana ikafanikiwa kutinga robo fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Misri
Nyota wa Stars sasa wanaelekea katika majukumu ya klabu zao