Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 1 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Feb 2024
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 1 2024

Aston Villa imemsajili mshambuliaji Morgan Rogers kutoka Middlesbrough kwa mkataba unaoripotiwa kuwa wa takriban £15m. Rogers, 21, amefunga mabao saba na kutoa asisti tisa katika michezo 33 aliyoichezea klabu hiyo ya Championship msimu huu

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 20 alihamia Riverside Stadium kutoka Manchester City kwa £1.5m kwa mkataba wa miaka minne Julai iliyopita. Middlesbrough ilikataa ofa tatu kutoka kwa Aston Villa kabla ya kukubaliana juu ya bei ya Rogers.

Mmiliki Steve Gibson alidhamiria kutomruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa chini ya hesabu yake - iliyofikiriwa kuwa karibu £12m. Manchester City pia walifanya mazungumzo ya ada ya mauzo ya 25% kutoka kwa faida ya mpango huo kwa Rogers, ambaye anacheza kama winga

Fulham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 22 kwa uhamisho wa dakika za lala salama (Evening Standard)

Chelsea wanataka pauni milioni 50 kwa Broja - bei ambayo Cottagers wanasita kuilipa (Mail)

Tottenham hawana uwezekano wa kufikia bei inayotakiwa na Chelsea ya pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anatazamiwa kusalia na The Blues kwa muda wote uliosalia.(Talksport)

Spurs wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa Uswidi mwenye umri wa miaka 17 Lucas Bergvall, anayechezea Djurgardens .(Football London)

Jose Mourinho, ambaye hivi majuzi alitimuliwa kama mkufunzi wa Roma , angetamani kurejea Manchester United kama meneja wa klabu hiyo ya Old Trafford iwapo nafasi hiyo itatokea.. (Mail)

Mkufunzi wa Bournemouth Andoni Iraola hatarajii mshambuliaji wa Uingereza Dominic Solanke kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhusishwa na Tottenham. (Evening Standard)

Aston Villa wamekubali dili la kumsaini beki wa pembeni wa England chini ya miaka 19 Lino Sousa, 19, kutoka Arsenal . (Fabrizio Romano)

Wolves wako kwenye mazungumzo juu ya uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji wa Corinthians na Brazil Yuri Alberto , 22 . (Telegraph - usajili unahitajika)

Brighton wako kwenye mazungumzo ya kumleta winga wa Uhispania Bryan Gil, 22, kwa klabu hiyo kwa mkopo kutoka Tottenham. (Evening Standard)

Stuttgart wanashinikiza kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Mahmoud Dahoud, 28, kutoka Brighton. (Sky Germany)

Sheffield United wamewasiliana na Leicester City kuhusu uhamisho wa mlinzi wao raia wa Australia Harry Souttar, 25, huku Blades wakijaribu kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Football Insider)

Everton pia wanamtazama Souttar, ambaye yuko na kikosi cha Australia kinachoshiriki Kombe la Asia nchini Qatar.. (Football League World)

Crystal Palace wanafikiria kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27 Maxwel Cornet, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka West Ham. (Telegraph - usajili unahitajika)

Aberdeen wanawezakumteua Neil Warnock mwenye umri wa miaka 75 kama meneja hadi mwisho wa msimu huu kufuatia klabu hiyo kumfukuza kazi Barry Robson (The Press and Journal)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’