International - Local

Eto matatani FIFA

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Feb 2024
Eto matatani FIFA

Rais wa Chama cha soka cha Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto'o ametuhumiwa kuhusika na upangaji wa matokeo na kutoa vitisho, katika faili la kustusha lililowasilishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Fifa

Kwa mujibu wa gazeti la The Athletic, Eto'o anakabiliwa na orodha ndefu ya tuhuma zilizoelekezwa kwake zikiwamo kuhusika katika upangaji wa matokeo, kusambaza taarifa za uongo, kutoa vitisho, kusababisha vurugu na matumizi mabaya ya madaraka

Makamu wa rais wa zamani wa Fecafoot, Henry Njalla Quan Junior amelituma faili hilo kwa Fifa na pia linachunguzwa na Caf

Shirikisho hilo la soka la Afrika pia limethibitisha kuwa linachunguza kuhusiana na madai hayo dhidi ya Eto'o na Fifa iliwahi kushauriwa kumtoa staa huyo wa zamani wa Barcelona katika nafasi yake kutokana na mfululizo wa matukio tata

Njalla Quan Junior amedai kwamba mechi kati ya akademi yake na Kumba City FC ilipangwa matokeo na Eto'o, akieleza tukio hilo kama moja ya 'kashfa kubwa kabisa maishani'

Bosi huyo wa Cameroon pia anatuhumiwa kupanga matokeo ya timu ya 'rafiki yake wa karibu' Valentine Nkwain ipande daraja

Victoria United ikapanda daraja baada ya kushinda mechi 11 kati ya 17 za mwisho wa msimu licha ya kupoteza mechi nne kati ya saba za kwanza za msimu huo

Gazeti la The Athletic likaongeza kuwa uhusiano wa Njalla Quan Junior na Eto'o uliharibika kabisa, na ukasababisha straika huyo wa zamani kudaiwa kumlipa mtu atume meseji ya vitisho iliyosomeka: "Mimi ni mafia wa mapinduzi haya na katika umafia huu hatuwasaliti viongozi wetu. Nimekuwa nikilinda maslahi ya mipango yetu hadi leo. Hivyo, kama utanizingua kaa tayari kubeba mzigo wa kitakachotokea"

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’