Simba kuendeleza ubabe ligi kuu leo?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Feb 2024
Simba kuendeleza ubabe ligi kuu leo?

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi nyingine ya kiporo kupigwa mkoani Tabora ambao wenyeji Tabora United wataikaribisha Simba katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Baada ya kuzoa alama tatu mkoani Kigoma katika mchezo dhidi ya Mashujaa Fc, Wekundu wa Msimbazi leo wataingia dimba la Ali Hassan Mwinyi wakiwa na malengo yaleyale ya kuvuna alama tatu

Kikosi cha kocha Abdelhak Benchikha kilitua Tabora juzi usiku na jana kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Ni wazi mchezo utakuwa mgumu, Tabora United wamejipambanua kuwa moja ya timu ngumu msimu huu hasa wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani

Katika mkutano na wanahabari jana, Kocha Msaidizi wa Simba Seleman Matola alisema wanafahamu aina ya mechi wanakwenda kukabiliana nayo leo, wamejipanga na watahakikisha wanavuna alama zote tatu

Ushindi dhidi ya Tabora United leo utaisogeza Simba karibu zaidi na waliojuu kwenye msimamo wa ligi

Simba inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 26, Azam Fc wako nafasi ya pili wakiwa na alama 31 na Yanga wanaongoza wakiwa na alama 34. Hata hivyo Simba ina mechi mbili za viporo

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’