Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anasema hakuna uamuzi ambao umefanywa kuhusu hatima ya beki wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 36, au beki wa kati wa Ufaransa Raphael Varane, 30. (Express)
Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27, lakini inasema ana thamani ya pauni milioni 70 hivyobasi haitajihusisha na ushindani wa kutaka kumsajili. (Star)
Rais wa La Liga Javier Tebas anasema kuna uwezekano wa kati ya 55-60% Real Madrid kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, kutoka Paris St-Germain msimu huu. (Mirror)
Liverpool wako tayari kutoa changamoto kwa Arsenal kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, kutoka Real Sociedad. (Football Transfers)
Klabu ya Saudi Arabia Al Ittihad itajaribu tena kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 31, msimu huu wa joto, baada ya kushindwa katika ombi la msimu uliopita. (ESPN)
Arsenal wamekuwa wakimfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 21. (Mirror) Kiungo wa kati wa The Gunners raia wa Ghana Thomas Partey, 30, anavutiwa na Juventus. (Fichajes – In Spanish)
Real Madrid inamfuatilia beki wa kushoto wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester City na Liverpool. (HITC)
Newcastle United wanamtaka kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 22. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 35, ana mkataba na Barcelona ambao utaendelea hadi Juni 2026 na anataka kuutimiza. (Sport – In Spanish)
Liverpool haitarajii kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 32, kusalia katika klabu hiyo zaidi ya msimu ujao. (Football Insider)
AC Milan wanatazamiwa kuwa miongoni mwa timu kadhaa za Italia kuonyesha nia ya kumnunua beki wa Arsenal na Poland Jakub Kiwior, 23, msimu ujao. (Evening Standard)
Blackburn Rovers wanatarajiwa kumteua meneja wa zamani wa Birmingham John Eustace kuchukua nafasi ya Jon Dahl Tomasson kama meneja mpya wa klabu hiyo ya Championship. (Mail)
Beki wa Uswidi Emil Krafth, 29, anatarajiwa kusaini mkataba wa kuongezwa katika klabu ya Newcastle. (FotbollDirekt – In Swedish)
BBC