Usiku wa kuamkia leo, Sebastien Haller alikuwa shujaa wa Ivory Coast wakati The Elephants walipotoka nyuma na kuwashinda Nigeria mabao 2-1 na kushinda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 wakiwa nyumbani
Mshambulizi huyo, ambaye pia alifunga bao la ushindi wa nusu fainali, aliunganisha krosi ya Simon Adingra zikiwa zimesalia dakika tisa kukamilisha mchezo huo kipindi cha pili na kuibua shangwe kali jijini Abidjan
William Troost-Ekong alikuwa ameiweka Nigeria mbele dakika saba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza wakati beki huyo wa kati aliporuka juu zaidi na kufunga kwa kichwa
Franck Kessie alifunga bao la kusawazisha dakika ya 62 kutokana na kona ya Adingra ambaye alitajwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa michuano hiyo
Ivory Coast haikuwa na mwanzo mzuri katika michuano hiyo ikipenya hatua ya 16 kupitia 'best looser' lakini baadae kila kitu kikabadilika hadi kuwa mabingwa
Ivory Coast walinyakua taji la tatu la bara na ushindi waliosatahili kuupata