Kikosi cha Simba leo kinashuka uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Baada ya kuangusha alama mbili kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopita, Simba leo haihitaji matokeo mengine tofauti na ushindi
Vijana wa kocha Abdelhak Benchikha wanafahamu matokeo mengine tofauti na ushindi yatazidi kuongeza presha katika mbio za ubingwa
Simba inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 30 lakini ina mechi mbili za viporo ambazo kama watashinda zote watafikisha alama 36 na kuwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga kwa tofauti ya alama nne tu
Azam Fc wako nafasi ya pili sasa wakiwa na alama 32 pia wana mchezo mmoja wa kiporo ambao kama watashinda watafikisha alama 35
Mchezo utapigwa kuanzia saa 10 jioni