Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa timu nyingi za Premier League zinazomtaka kiungo wa kati wa Atalanta Ederson, huku Arsenal, Newcastle na Tottenham pia zikimfuatilia Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport – in Itali)
Juventus pia wanampenda Ederson, lakini wababe hao wa Serie A wameamua kufanya usajili wa mchezaji mwenza wa Atalanta Teun Koopmeiners - kiungo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 - kuwa kipaumbele chao. (Gazzetta dello Sport – In Itali)
Liverpool wanavutiwa na beki wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi, 23. (Telegraph – Subscription Required)
Paris St-Germain inalenga mshambuliaji wa Napoli mwenye umri wa miaka 25 Victor Osimhen, mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 26 na kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 19 Gavi msimu huu. (I)
Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Juventus na Brazil mwenye umri wa miaka 26 Gleison Bremer, ambaye thamani yake ni euro 70m (£59.8m). (Calciomercato – In Itali)
Makamu mwenyekiti wa Fulham Tony Khan anasema klabu itazingatia ofa ambazo "zina maana" kwa kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28. (Sports)
Manchester United wanafikiria kurejesha hamu yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane mwenye umri wa miaka 30 na kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 26, msimu huu. (Football Transfers)
Aston Villa wanajiandaa kufungua zabuni ya kumnunua kiungo wa Red Bull Salzburg Oscar Gloukh - Misraeli mwenye umri wa miaka 19 ambaye pia amevutia Manchester United, Arsenal, Liverpool, Newcastle United na Barcelona - kwa ofa ya euro 20m (£. 17m). (Ekrem Konur)
Sheffield Wednesday, Bolton Wanderers na Peterborough United wanachunguza kumnunua kiungo wa kati wa Jamaica Ravel Morrison, 31, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka DC United ya MLS. (TeamTalks)
BBC



