Jana Simba ilivuna alama moja muhimu nchini Ivory Coast baada ya kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Asec Mimosas katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika
Ulikuwa mchezo wa vipindi viwili Asec wakiwa bora katika kipindi cha kwanza huku Simba wakitawala kipindi cha pili
Pengine Sadio Kanoute atajilaumu kwa kukosa nafasi muhimu ya kuifungia Simba bao mapema katika kipindi cha pili
Sio matokeo mabaya kwa Simba kwani sasa ushindi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, utaihakikishia Simba kutinga robo fainali
Asec Mimosas wamejihakikishia kumaliza nafasi ya kwanza kundi B baada ya suluhu dhidi ya Simba
ADVERTISE HERE