Simba - Local

Simba yaapa kulipa kisasi dhidi ya Jwaneng Galaxy

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Feb 2024
Simba yaapa kulipa kisasi dhidi ya Jwaneng Galaxy

Kikosi cha Simba kimerejea Tanzania usiku wa kuamkia leo wakitokea Ivory Coast walikofanikiwa kupata alama moja muhimu katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asec Mimosas uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Akizungumza muda mfupi baada ya timu kutua JNIA, Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola alisema akili na mahesabu yao wanayaelekeza kwenye mchezo wa Machi 2 dhidi ya Jwaneng Galaxy

Simba inahitaji kushinda mchezo huu ili iweze kutinga robo fainali ya tano katika miaka sita

"Tulihitaji kushinda mchezo dhidi ya Asec lakini naweza kusema tulikosa bahati lakini vijana walipambana nafikiri wote mliona" alisema Matola na kuongeza,

"Tunakwenda kufanya maandalizi kuelekea mchezo wetu wa mwisho ambao kwetu ni kama fainali, kuna mambo mawili katika mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy kutafuta ushindi utakaotupeleka hatua ya robo fainali na kulipa kisasi"

"Hii haitakuwa mechi ya kawaida bali ni fainali kwetu kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kwenda robo fainali," alisema Matola.

Simba haitakuwa tayari kurudia makosa ya msimu wa 2020/2021 kwa kupoteza nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy na kukosa nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa na badala yake kuangukia katika kombe la Shirikisho ambako walifanikiwa kufika robo fainali

Simba itahitaji ushindi wa aina yoyote kutinga robo fainali pasipo kujali matokeo ya mchezo kati ya Wydad dhidi ya Asec

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
5h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
9h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
13h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
15h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
16h ago
READ MORE β†’