Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Februari 27 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Feb 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Februari 27 2024

Real Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili beki wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, na watatarajia kukamilisha dili hilo msimu huu wa joto au 2025, atakapokuwa mchezaji huru. (Athletic- Usajili unahitajika)

Mustakabali wa kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino haujulikani baada ya timu yake kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool, huku kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim akitarajiwa kuchukua nafasi yake. (Mail)

Manchester United inatarajiwa kuwatoa wachezaji kadhaa msimu huu huku winga wa Brazil Antony, 24, akiwa miongoni mwa wale ambao watakuwa tayari kuwauza. (MEN)

Chelsea wanatumai kumuuza mlinzi Trevoh Chalobah, 24, na mshambuliaji wa Albania Armando Broja, huku mustakabali wa kiungo wa Uingereza Conor Gallagher, 24, na beki wa Uhispania Marc Cucurella, 25, ukiwa mashakani wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa msimu huu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)

Bayern Munich, Liverpool na Arsenal wako kwenye mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne angependelea kuhamia Major League Soccer (MLS) badala ya Ligi Kuu ya Saudi Pro. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anatimiza miaka 33 msimu huu wa joto, wakati mkataba wake unaingia mwaka wake wa mwisho. ( Athletic- Usajili unahitajika)

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 51, yuko tayari kufundisha nchini Italia, huku nyota huyo wa Ufaransa akihusishwa na kurejea Juventus. (La Gazzetta dello Sport kwa Kiitaliano)

Kipa wa England Aaron Ramsdale, 25, ana nia ya kuondoka Arsenal msimu wa joto baada ya kupoteza nafasi yake kwa kipa wa Uhispania David Raya, 28. (Football Insider)

Tottenham wanaongoza katika harakati za kumsaka mshambulizi wa Hull City Jaden Philogene, 22, ingawa Aston Villa wana kipengele cha kumnunua winga huyo wa chini ya miaka 21 wa England. (Teamtalk)

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Omari Forson,19, anaweza kuondoka Manchester United msimu huu wa joto, huku kiungo huyo mshambuliaji akimaliza mkataba wake Old Trafford. (Athletic- Usajili unahitajika)

Celtic wanatazamia kumnunua mlinda mlango wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 25, huku wakitafuta namba moja kwa msimu ujao. (Football Insider)

Beki wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, ana nia ya kurejea Barcelona licha ya kutakiwa na Manchester United. (90 min)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’