Wakati mashabiki wa Simba na Yanga wakiendelea na shamrashamra baada ya timu zao kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, mafanikio yao ni ya Tanzania
Kwa mara ya kwanza Tanzania imeingiza timu mbili katika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Hii itaongeza alama za Tanzania katika viwango vya CAF na kuwa na uhakika wa kutoa timu nne katika mashindano ya CAF kwa muda mrefu zaidi
Katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, ni Tanzania pekee iliyotoa timu mbili




