Azam - Yanga - Local

Manara ataka Dube achangiwe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2024
Manara ataka Dube achangiwe

Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara amewataka wadau wa soka kumchangia mshambuliaji Prince Dube ambaye ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba wake na matajiri wa Chamazi, Azam Fc

Manara amebainisha kuwa kama alivyochangiwa Feisal Salum katika jitihada zake za kuondoka Yanga basi Wananchi nao wamchangie Dube

"Wananchi naomba na sisi tumchangie Dube Prince kama alivyochangiwa Fei," aliandika Manara katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Jana klabu ya Azam Fc ilithibitisha kupokea barua ya Dube aliyeomba kuvunja mkataba wake ili akatafute changamoto sehemu nyingine

Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' alisema mkataba wa Dube na Azam Fc unamalizika mwaka 2026 lakini wako tayari kumuachia mchezaji huyo iwapo atafuata taratibu za kuvunja mkataba huo

Zakazakazi alisema gharama ya kuvunja mkataba uliobaki ni dola laki tatu (zaidi ya Mil 800) huku akitangaza watapokea ofa ya timu yoyote inayomtaka mchezaji huyo raia wa Zimbabwe

Hata hivyo baadhi ya wadau wa soka nchini wamewataka Azam Fc kuwa waungwana kwa Dube ambaye amewatumikia kwa moyo mmoja tangu alipojiunga nao mwaka 2020

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’