UEFA yaja na muundo mpya

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th March 2024


UEFA yaja na muundo mpya

Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limetangaza muundo mpya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2024/2025

Awali zilikuwa timu 32 na sasa zitaongezeka hadi 36. Kutakuwa na poti nne, kila timu itakuwa na michezo minne ya nyumbani na minne ugenini, hivyo kila timu itakuwa na michezo minane.

Timu ambazo zitamaliza nafasi ya 1-8 zitaenda moja kwa moja 16 bora, timu ambazo zitashika nafasi ya 9-24 zitashindana zenyewe kwenye mtoano

Timu zitakazoshika nafasi ya 25-36 zitaondolewa moja kwa moja kwenye mashindano


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.