Klabu ya Simba inaelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumatano March 06 katika uwanja wa Jamhuri
Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa raundi ya 16 utakaopigwa saa 10 jioni
Uongozi wa Simba jana ulitangaza kuwa mechi zote za nyumbani zilizobaki katika ligi kuu na kombe la FA, zitachezwa katika dimba la Jamhuri
Aidha Simba imeridhishwa na maboresho yaliyofanyika katika uwanja huo sasa ukiwa tayari