Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano March 06 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Mar 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano March 06 2024

Manchester United ilituma maskauti kumtazama mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee katika mchezo wao dhidi ya Atalanta siku ya Jumapili. (Tuttosport )

Arsenal pia wana nia ya kumsajili Zirkzee, ambaye anaweza kugharimu kama euro 80m (£68m). (Gazzetta dello Sport )

Manchester City wanajiandaa kuipiku Liverpool katika kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 29, msimu huu. (Caught Offside)

Liverpool wanavutiwa sana na winga wa Wolves Pedro Neto mwenye umri wa miaka 23, lakini wana wasiwasi kuhusu rekodi ya jeraha ya mshambuliaji huyo wa Ureno. (Football Insider)

Crystal Palace wanaandaa orodha ya wachezaji wanaolengwa wa nafasi ya mlinzi wa kati huku beki wa Uingereza Marc Guehi, 23, akitarajiwa kuuzwa msimu huu wa joto kwa ada ya zaidi ya £50m. (Telegraph)

Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim ndiye anayelengwa zaidi na Barcelona kurithi mikoba ya Xavi mwishoni mwa msimu huu, ingawa meneja huyo wa Ureno anaaminika pia kuwa na hamu ya kujiunga na Liverpool. (Independent)

Bayern Munich wanavutiwa na mlinzi wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha kati ya euro 40m (£34.2m) na euro 45m (£38.5m). (Sky Sports )

Newcastle wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 25 Lloyd Kelly kwa uhamisho wa bure. (Mail)

Barcelona itasikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Pedri, 21, msimu huu kwa sababu ya wasiwasi juu ya historia yake ya jeraha huku wakijaribu kusawazisha vitabu vyao. (AS )

Everton inamfuatilia mlinzi wa Hull City Jacob Greaves, 23, huku kukiwa na nia ya kumnunua beki wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21, kutoka Manchester United na Tottenham. (Mirror)

Vilabu vinne vya Premier League vinapigana vikumbo kumsaini Roony Bardghji wa Copenhagen mwenye thamani ya pauni milioni 20, huku Aston Villa, Newcastle, Tottenham na Manchester United zote zikimhitaji kiungo huyo wa kati wa Uswidi mwenye umri wa miaka 18. (HITC)

Klabu ya Hull inayoshiriki michuano hiyo ingependa kutafuta uhamisho wa kudumu kwa winga wa Liverpool aliyeko kwa mkopo Fabio Carvalho, 21, ikiwa watashinda kupanda Ligi ya Premia. (i sport)

Manchester United wanatarajiwa kuwasiliana na Crystal Palace kwa ajili ya mkurugenzi wao wa michezo Dougie Freedman mwenye umri wa miaka 49. (Guardian)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’