Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo Jumatano, March 06 ambapo mechi nne zitapigwa katika viwanja mbalimbali
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wako mkoani Morogoro kupepetana na Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Simba imehamisha makazi yake mkoani Morogoro kwa muda ambapo itatumia uwanja huo katika mechi za nyumbani za ligi na kombe la FA
Mashujaa Fc watachuana na JKT Tanzania katika mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 jioni
Azam Fc dhidi ya Coastal Union mechi itapigwa saa 12 jioni na mechi ya mwisho leo ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Tabora United saa 2:15 usiku
