Matajiri wa Chamazi, Azam FC jana walidhihirisha ubora wao mbele ya Yanga wakiibuka na ushindi wa 2-1 katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Yanga walianza mchezo huo kwa kupata bao la mapema, dakika 10 mfungaji akiwa Clement Mzize lakini furaha ya ilidumu kwa dakika tisa tu kabla ya mshambuliaji wa Gambia Gibril Sillah kusawazisha dakika ya 19
Dakika 51 Feisal Salum Abdallah ‘Feitoto’ akawainua vitini wanazi wa Azam FC akifunga bao la pili akiwaadhibu waajiri wake hao wa zamani
Hilo lilikuwa bao la 13 kwa Feisal ambaye anachuana na Stephane Aziz Ki katika mbio za ufungaji bora wote wakiwa na mabao 13
Ushindi huo uliiwezesha Azam Fc kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa wamevuna alama 47 katika michezo 21 huku Yanga wakiendelea kushika usukani wa ligi kwa jumla ya alama 52



