Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekiri kikosi chake hakikuwa katika ubora na hivyo kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana
Hata hivyo Gamondi amesema mazingira ya mchezo huo yalikuwa magumu kwa upande wao
Gamondi amelalamika ugumu ya ratiba ambayo wachezaji wake wamekumbana nayo kabla ya mchezo huo
"Tumecheza mechi tano katika kipindi kifupi, hawa wachezaji ni binadamu sio roboti"
"Bao la kwanza tulifungwa kutokana na makosa yetu lakini bao la pili kulikuwa offside ya wazi wazi"
"Sisi hatulalamiki kufungwa lakini nadhani kuna mazingira hatukutendewa haki katika mchezo huu. Najua kuna watu wamefurahi leo baada ya mechi hii...!," alisema Gamondi
Katika mchezo huo ambao Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-1, wachezaji Pacome Zouzoua na Yao Kouassi walishindwa kumaliza mchezo baada ya kupata majeraha
Pacome aliumizwa goti katika dakika 30 wakati Yao alipata majeraha ya misuli wakati mchezo huo ukielekea ukingoni
Wachezaji hao wanatarajiwa kufanyiwa vipimo kubaini ukubwa wa majeraha yao na pengine kama ni majeraha makubwa linaweza kuwa pigo kwa Yanga kuelekea mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa March 30



