Yanga - Simba - Azam - Local

Ujio wa Al Hilal Ligi Kuu ya NBC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2024
Ujio wa Al Hilal Ligi Kuu ya NBC

Wadau wa soka nchini wamepokea kwa mtazamo tofauti ujio wa klabu ya Al Hilal kushiriki ligi kuu ya NBC msimu ujao

Bodi ya Ligi imethibitisha kupokea maombi ya Al Hilal kushiriki ligi kuu ya NBC msimu ujao kutokana na vita inayoendelea huko Sudan iliyosababisha shughuli zote za michezo kusimama kwa takribani miaka miwili sasa

Taarifa kutoka ndani ya TFF zimethibitisha kuwa Al Hilal wamekubaliwa kushiriki ligi kuu msimu ujao lakini hawatakuwa kwenye msimamo wa ligi na ambapo pointi watakazo kusanya hazitahesabiwa

Kwa maana mechi zao zitakuwa kama za kirafiki tu kwani hazitakuwa athari yoyote kwa timu nyingine kwenye ligi

Baadhi ya wadau wametoa maoni yao wakiamini ujio wao utakwenda kuongeza idadi ya mechi ambazo timu zitapaswa kucheza pasipo na faida yoyote

"Hapa tunakwenda kuziongezea timu mechi pasipo na faida yoyote. Naamini hata klabu hazitachukulia mechi dhidi ya Al Hilal kwa uzito kwa sababu ni kama mechi za kirafiki tu"

"Mimi naona kama kuna ulazima wa Al Hilal kushiriki ligi yetu basi nao wawemo kwenye msimamo. Kitu pekee ambacho hawapaswi kunufaika nacho ni nafasi za ushiriki wa ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho," alisema Ifraim Masoud kutoka mkoani Mbeya

Nae mchambuzi wa soka Hans Rafael amesema pamoja na alama za timu hiyo kutohesabiwa katika msimamo lakini bado zitahesabiwa 'vijiweni' na italeta mijadala mwishoni mwa msimu kama itatokea wamepata alama nyingi kuliko timu itakayokuwa bingwa

"Sasa ikitokea  wamekusanya pointi nyingi kuliko timu zote na kombe akapewa mtu wa pili kikanuni huu ubingwa utakuwa na mvuto kweli? Na kwa utani wa Simba na Yanga bingwa atapata nguvu ya kutamba?"

Mkurungezi wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo amesema ujio wa Al Hilal inawezekana kwa sababu ni jambo ambalo linazungumzika kutokana na hali ya kiusalama nchini Sudan kwa sasa

Kasongo ameongeza kuwa kama Al Hilal watashiriki ligi msimu ujao faida ni nyingi kwa klabu za Tanzania kuliko chagamoto kutokana na uzoefu wa timu hiyo kushiriki mara kwa mara michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho

Pia amesema kuna baadhi ya waamuzi kutoka Sudan watakuwa miongoni mwa watakochezesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao 2024/2025.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’