Newcastle United wanafikiria kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, ili kufadhili matumizi yao ya msimu wa joto. (Football Insider)
Real Madrid na Paris St-Germain walikuwa wakimtazama Guimaraes katika kichapo cha Jumamosi cha Kombe la FA dhidi ya Manchester City, huku PSG pia wakifuatilia kwa karibu mmoja wa wachezaji wenzake wa Newcastle - mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24. (HITC)
Bayern Munich wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anataka tu kujiunga na Manchester City, Arsenal, Liverpool, Real Madrid au Barcelona. (Florian Plettenberg)
Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazotaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Morocco Brahim Diaz, 24. (HITC)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva anasema ana uhakika atarejea katika klabu yake ya kwanza ya Benfica, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikataa kusema lini. (SIC - via Portugal)
Everton itahitaji kima cha chini cha pauni milioni 80 kumnunua mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, ambaye anasakwa na Manchester United na Chelsea. (Team Talks)
Mshambulizi wa Uingereza Raheem Sterling, 29, atakataa nia ya Saudi Arabia msimu huu wa joto huku akijaribu kushinda medali na Chelsea msimu ujao. (Standard)
Chelsea wanatazamia kumzawadia fowadi wa Uingereza Cole Palmer, 21, mkataba mpya na masharti yaliyoboreshwa baada ya kuanza maisha vizuri Stamford Bridge. (Football Insider)
&Eddie Nketiah huenda akaondoka Arsenal msimu huu wa joto na Wolves wamejiunga na vilabu vya Ligi ya Premia wakiwinda uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza, 24. (Teamtalk)
Tottenham Hotspur wameelekeza macho yao kwa beki wa pembeni wa West Ham Muingereza Ben Johnson, 24. (Football) Liverpool wameongeza hamu yao ya kumnunua beki wa upande wa kushoto wa Bayer Leverkusen Piero Hincapie, mchezaji wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 22. (HITC)
Manchester United wako kwenye mazungumzo ya juu na kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18, kuhusu kandarasi mpya. (Football Insider)
Chelsea wamemtambua kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi kama mbadala wa kocha wao wa sasa Mauricio Pochettino. (TeamTalks)
Mshambulizi wa zamani wa Manchester United Eric Cantona amedokeza kuwa atavutiwa na nafasi katika klabu hiyo chini ya mmiliki mpya wa sehemu Sir Jim Ratcliffe. (Independent)
BBC



