Simba - Ahly - Local

Simba yapania ushindi mnono dhidi ya Al Ahly

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Mar 2024
Simba yapania ushindi mnono dhidi ya Al Ahly

Simba iko kwenye maandalizi kabambe visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly

Mnyama amepania kukivuka kiunzi cha robo fainali ambacho amekwana katika misimu minne

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisisitiza umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingu uwanja wa Benjamin Mkapa March 29 huku akiweka wazi dhamira ya Simba kutinga nusu fainali

Ahmed alibainisha kuwa mkakati wa Simba ni kupata ushindi mnono nyumbani ili kujiweka katika nfasi nzuri ya kutinga nusu fainali

"Safari hii tunataka kupata ushindi mkubwa wa kutupeleka nusu fainali, tukishinda goli nyingi Uwanja wa Mkapa tukienda kwao hata tucheze siku tatu hawatakuwa na uwezo wa kupindua matokeo"

"Tarehe 29 ni siku ya kufa na kupona, siku ya kupambania Simba yetu. Tujitahidi kila Mwanasimba aje Uwanja wa Mkapa. Tuhamasishane kwenye matawi, kwenye makundi, kwenye mitaa ili tarehe 29 tukutane Uwanja wa Mkapa"

"Mechi yetu ni saa 3 usiku hivyo una option ufturu nyumbani ndio uje uwanjani, au uje Uwanja wa Mkapa utafturu huko huko, futari itauzwa nje ya uwanja alafu ndio uingie uwanjani. Huna sbabau yoyote ya kutokuja uwanjani siku hiyo"

"Tupo kwenye mazungumzo na Jeshi la Polisi ili kuwe na ruti ya magari kuja moja kwa moja uwanjani. Tunaongea nao pia usalama uwe madhubuti ili Wanasimba waje uwanjani na waondoke uwanjani kwa usalama. Uzuri tunae Afande Mudi ni Mkuu wa Kituo cha Chang’ombe ambaye atahakikisha Mwanasimba hapati madhara yoyote"

"Wewe mwenyewe hapo ulipo jiambie unatakiwa kwenda uwanjani, weka nia. Na tiketi zimeanza kuuzwa, hii ni mara ya kwanza tiketi kuanza kuuzwa wiki moja na nusu kabla kutokana na umuhimu na uhitaji wa tiketi kwa Wanasimba," alisema Ahmed

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’