Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi April 11 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Apr 2024
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi April 11 2024

Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, ambaye atagharimu hadi £40m msimu huu wa joto. (Florian Plettenberg)

Wakala wa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres anasema itakuwa vigumu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusalia Sporting Lisbon ikiwa meneja Ruben Amorim, ambaye anahusishwa na Liverpool, ataondoka katika klabu hiyo. (A Bola - kwa Kireno)

Meneja wa Lille, Paulo Fonseca anaongoza orodha ya wanaozingatiwa na West Ham kuchukua nafasi ya umeneja ikiwa The Hammers wataachana na David Moyes katika majira ya joto. (I) Chelsea inamlenga mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, msimu huu wa joto lakini klabu hiyo itahitaji kwanza kuuza wachezaji ili kupata fedha.(Football Transfers)

Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino na makocha wake hawajafurahishwa na mchezo wa fowadi wa Ukraine Mykhaylo Mudryk mwenye umri wa miaka 23 msimu huu na The Blues watakuwa sokoni kutafuta winga mpya msimu huu. (Football Insider)

Bayer Leverkusen wameungana na Liverpool na Tottenham katika harakati za kumsajili winga wa Leeds United Mholanzi Crysencio Summerville, 22. (Bild via Teamtalk)

Aston Villa wanazidi kuwa na matumaini kuwa kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 25, atasaini mkataba mpya wa muda mrefu. (Talksport)

Shakhtar Donetsk wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ukraine Georgiy Sudakov, huku Liverpool, Aston Villa, Arsenal na Manchester City wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (HITC)

Beki wa Inter Milan Denzel Dumfries anaweza kuwa analengwa na Aston Villa na klabu hiyo ya Italia itazingatia ofa ya zaidi ya euro 30m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 27, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Serie A unamalizika 2025. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester United itawaacha wachezaji 12 wa kikosi chao cha kwanza kuondoka Old Trafford katika hatua ambayo itakuwa kubwa katika kuunda timu mpya ya klabu hiyo msimu huu wa joto. (FourFourTwo)

Kipa wa Ujerumani Alexander Nubel, 27, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na Bayern Munich ambao utahusisha kuendeleza mkataba wake wa mkopo na Stuttgart kwa msimu mwingine. (Bild)

Washirika wa 777, mwekezaji anayejaribu kuchukua udhibiti wa Everton, ameahirisha tarehe iliyolengwa ya kukamilisha mpango huo huku ikijaribu kukusanya mamia ya mamilioni ya pauni kuufadhili.(Sky News)

Makubaliano yameafikiwa kwa mkufunzi wa Lyon Sonia Bompastor kuwa meneja ajaye wa klabu ya Chelsea ya Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu akirithi mikoba ya Emma Hayes. (Telegraph - usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’