Azam - Namungo - Local

Azam Fc yaipania Namungo Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Apr 2024
Azam Fc yaipania Namungo Fc

Klabu ya Azam Fc imepania kulipa kisasi dhidi ya Namungo kutokana na kupoteza mechi ya nyumbani ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Oktoba 27, mwaka jana Azam ikiwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Namungo

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Azam, Thabit Zacharia, alisema moja kati ya mechi muhimu zaidi msimu huu kwao katika Ligi Kuu Bara ni dhidi ya Namungo itakayochezwa Jumapili mkoani Lindi

Zaka alisema mbali na kuhitaji pointi tatu kutokana na vita kali iliyopo juu kati yao na vigogo, Simba na Yanga, lakini wanahitaji kulipiza kisasi kwa sababu hawaelewi sababu iliyofanya wakafungwa katika mechi wa kwanza

"Ni mchezo muhimu kwetu japo tupo juu ya Simba, lakini tuko huko kwa sababu tumecheza michezo mingi zaidi, hivyo hatutakiwi kupoteza michezo iliyobaki, hatutakiwi kuangusha pointi zaidi kwa sababu kuna wenzetu tumewazidi lakini wana michezo michache"

"Halafu kisasi ni haki, tunakwenda kulipiza kisasi kwa sababu mchezo wa kwanza walitufunga hapa kwetu Azam Complex," alisema Zaka Zakazi

Azam FC inakwenda kucheza mechi hiyo ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo, ikiwa na pointi 47, nyumba ya Yanga inayoongoza kwa pointi 52 na juu ya Simba iliyo nafasi ya tatu yenye pointi 45. Hata hivyo, Azam imecheza mechi mbili zaidi ukilinganisha na Simba, ikiwa imeshuka dimbani michezo 21, Wekundu wa Msimbazi wakicheza mechi 19 mpaka sasa.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
2h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
6h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
7h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
8h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
9h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
22h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’