Yanga ilivyoimaliza Simba kibabe kwa Mkapa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Apr 2024
Yanga ilivyoimaliza Simba kibabe kwa Mkapa

Mechi ya watani wa jadi, iliyochezwa juzi, Uwanja wa Benjamin Mkapa, iliyomalizika kwa Yanga kuifunga Simba mabao 2-1, imeacha rekodi kadhaa ikiwamo mabao yote matatu kufungwa kwa mguu wa kushoto

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mzunguko wa pili, mabao yote yalifungwa katika lango la Kusini na wachezaji wa kigeni watupu, huku Waivory Coast wawili, Joseph Guede wa Yanga na Freddy Michael, waliosajiliwa kipindi cha dirisha dogo, wakiweka rekodi ya kufunga mabao katika dabi zao za kwanza nchini

Kiungo mshambuliaji wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, aliingia kwenye rekodi ya kufunga mabao kwenye mechi zote mbili za msimu mmoja, akiifikia rekodi ya Amissi Tambwe aliyefanya hivyo msimu wa 2015/16

Alifunga bao moja katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Novemba 5, mwaka jana, kwenye uwanja huo huo, akiiongoza timu yake kushinda mabao 5-1. Aziz Ki, pia ameendeleza rekodi yake nzuri ya kuifunga Simba, kwani hata msimu uliopita alifanya hivyo katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika mchezo wa dabi uliochezwa, Oktoba 23, 2022, na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1, kabla ya Simba kuifunga Yanga mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa pili iliyochezwa Aprili 16, 2023

Baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi na Hussein Kazi ndani ya eneo la hatari, Aziz Ki, raia wa Burkina Faso alifunga bao hilo kwa kutumia mguu wa kushoto dakika ya 19, kabla ya Guede kupachika la pili dakika ya 37, alipopokea mpira mrefu uliopigwa kutoka katikati ya uwanja, akaumiliki peke yake mabeki wa Simba wakidhania kuwa ameotea, akamlamba chenga kipa Lakred kabla ya kuujaza wavuni

Freddy alipachika bao la kufutia machozi kwa mguu wa kushoto dakika ya 73, akiitendea haki pasi ya Clatous Chama, akiwalambisha sakafu, Ibrahim Hamad 'Bacca' na Bakari Mwamnyeto, kabla ya kuukwamisha wavuni

Mechi ya juzi imemfanya Aziz Ki, kuendelea kuongeza pengo la ufungaji katika Ligi Kuu baina yake na Feisal Salum wa Azam FC, akifikisha mabao 15, ingawa Feisal Salum nae alijibu mapigo kwa kufunga bao pekee la Azam Fc katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu Fc

Yanga imerudia rekodi yake iliyoiweka msimu wa 2015/16 kuifunga Simba mara mbili kwa msimu mmoja, ambapo ilikuwa mara ya mwisho kwa mechi za dabi timu moja kushinda mara hizo kwa msimu mmoja

Mechi ya mzunguko wa kwanza ilishinda mabao 2-0, yaliyowekwa wavuni na Amissi Tambwe na Malimi Busungu na mzunguko wa pili ilishinda idadi hiyo hiyo ya mabao yaliyofungwa na Donald Ngoma na Tambwe

Matokeo ya mechi hiyo yameifanya Yanga kuukaribia ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa imefikisha pointi 58, ikicheza mechi 22 na kusalia na michezo minane ikiendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo Ligi Kuu, huku Simba iliyocheza michezo 21 mpaka sasa, ikisalia na pointi zake 46, ikiwa nafasi ya tatu, ikibakisha michezo tisa kabla ya kuhitimisha mechi zake za msimu huu

IPP Media

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
3h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
3h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
3h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
6h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
18h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
20h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
22h ago
READ MORE β†’