Siku moja baada ya kuachana na kocha Abdelhak Benchikha Simba inarudi uwanjani leo kuchuana na Namungo ya Lindi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, Simba ikiwa ugenini
Kwa mara nyingine leo kikosi kitakuwa chini ya kocha wa Juma Mgunda ambaye atasaidiana na Seleman Matola
Matola alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la kocha Benchikha ambaye mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Namungo Fc aliishuhudia ikimalizika kwa sare ya bao 1-1 pale uwanja wa Uhuru
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikisaka ushindi wa 15 msimu huu, ushindi ambao utawafanya wafikishe pointi 49 na kuendelea kuisogelea Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 54 na Yanga iliyopo kileleni na alama 62
Mgunda atakuwa na jukumu la kuirejesha Simba katika mbio za ubingwa na hatahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi leo
Uzuri idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi cha Simba alifanya nao kazi msimu uliopita ni wachezaji wachache tu ambao atakuwa akifanya nao kazi kwa mara ya kwanza
Jana Mgunda alisimamia mazoezi ya mwisho katika dimba la Majaliwa ambapo baada ya mazoezi hayo alisema amewaelekeza wachezaji nini wanapaswa kufanya katika mchezo dhidi ya Namungo