Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne April 30 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Apr 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne April 30 2024

Liverpool wanatarajia Mohamed Salah atasalia katika klabu hiyo na wanataka mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Misri mwenye umri wa miaka 31 kuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao. (The Athletic-Usajili unahitajika)

Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool ajaye, Richard Hughes ataongoza mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa Salah, ambaye mkataba wake wa sasa utaendelea hadi 2025. (Times - usajili unahitajika)

Marcus Rashford atakabiliwa na mtihani wa kuamua klabu atakayohamia iwapo ataamua kuondoka Manchester United, huku Paris St-Germain wakisitisha nia yao ya kumnunua mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 26.

Beki wa Crystal Palace mwenye thamani ya pauni milioni 55 kutoka Uingereza Marc Guehi, 23, ananyatiwa na Liverpool huku klabu hiyo ikimtafuta mbadala wa mlinzi wa Cameroon Joel Matip, 32, ambaye anatazamiwa kuondoka mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Football Insider)

Ajax wana nia ya kumteua tena Erik ten Hag kama kocha wao iwapo ataondoka Manchester United msimu huu wa joto. (Mail)

Nia ya West Ham kumnunua mkufunzi wa zamani wa Uhispania Julen Lopetegui imesitishwa baada ya kujua kwamba AC Milan ina mashaka kuhusu kumteua kama mbadala wa Stefano Pioli. (Guardian)

The Hammers pia wanataka kuwasajili winga wa Coventry Callum O'Hare mwenye umri wa miaka 25 na mlinzi wa Hull Muingereza Jacob Graves msimu huu wa joto. (Guardian)

Leicester wataweza kuwasajili wachezaji wakati dirisha la usajili la majira ya kiangazi litakapofunguliwa licha ya kuwekewa vikwazo na Ligi ya Soka ya Uingereza. (Mail) Hata hivyo, Foxes watalazimika kuwauza wachezaji kabla ya Juni 30 ili kuepuka malipo ya sheria ya faida na uendelevu (PSR)

msimu ujao huku kiungo wa kati wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 25, akiwaniwa na Brentford, Brighton na Fulham. (Mail)

Manchester United bado wanapanga kumteua Dan Ashworth kama mkurugenzi wa michezo msimu huu huku wakitarajia kwamba makubaliano ya kulipwa fidia na Newcastle yatakubaliwa hivi karibuni. (Football Insider)

Mshambulizi wa zamani wa Uingereza Jermain Defoe, 41, huenda akapata nafasi yake ya kwanza ya umeneja baada ya kufanya mazungumzo na klabu ya zamani ya Sunderland. (Sun)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’