Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, May 04 2024

Joel JJ By Joel JJ
4 May 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, May 04 2024

Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel ni miongoni mwa orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag iwapo Mholanzi huyo ataondoka msimu wa joto. (Times)

Lakini Tuchel amefungua milango ya kusalia Bayern Munich baada ya msimu huu licha ya kutangazwa Februari kwamba ataondoka. (Florian Plettenburg)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amemfanya mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 24, kuwa shabaha yake kuu msimu huu wa joto. (Independent)

Arsenal wameanza mazungumzo ya kandarasi na mlinzi wa kati wa Brazil Gabriel, 26, katika jitihada za kupigana na klabu kubwa za Ulaya. (Football Insider)

Makamu wa rais wa Inter Milan Javier Zanetti amependekeza kuwa mabingwa hao wa Serie A huenda wakashindana na Manchester United na Arsenal katika kuinasa saini ya mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Manchester United imefanya mawasiliano na wakala wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye mkataba wake na Juventus unakamilika msimu huu wa joto. (Team Talk)

Mlinzi wa kati wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, anaelekea kujiunga na Newcastle mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Mail)

Everton wanatumani ya kumshawishi Jarrad Branthwaite, 21, kusalia Goodison Park kwa mwaka mmoja zaidi lakini Manchester United wana imani kwamba dau la £60-70m kwa beki huyo wa kati wa Uingereza litakubaliwa. (Football Insider)

Tottenham itasikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 26 msimu huu wa joto. (Telegraph)

Real Madrid imefanya uchunguzi kwa River Plate kuhusu kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa chini ya miaka 20, Franco Mastantuono, 16. (Fabrizio Romano)

Barcelona wamemfanya kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 30, kuwa mlengwa wao mkuu katika usajili msimu huu. (Caught offside)

Manchester City wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Lazio Christos Mandas, huku Manchester United pia ikimtaka mlinda mlango huyo wa Ugiriki mwenye umri wa miaka 22. (Corriere dello Sport)

Inter Miami wako kwenye mazungumzo ya kumleta kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid na Argentina Angel Di Maria, 36, kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Soka. (ESPN Argentina)

BBC

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
54m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
57m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →