Simba bado ina matumaini ya kumbakisha Kibu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th May 2024


Simba bado ina matumaini ya kumbakisha Kibu

Bado Simba ina matumaini ya kumshawishi kiungo mshambuliaji Kibu Denis kusaini mkataba mpya kuendelea kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi

Habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimethibitisha kuwa wiki ijayo, watakutana na wakala wa Kibu ili kumaliza mvutano uliopo juu ya mkataba mpya

Kibu bado hajasaini mkataba aliopatiwa na Simba akitaka dau nono zaidi ambalo hata hivyo kiuhalisia anaweza kukwama kwani kiasi cha Tsh Milioni 500 alizohitaji ni fedha nyingi sana kwa mkataba wa miaka miwili

Wakati Kibu anasajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita kutoka klabu ya Mbeya City, Simba ilitumia Tsh Milioni 200 kumsajili ambapo sehemu ya fedha hizo ililipwa Mbeya City ambayo ilikuwa bado ina mkataba wa mwaka mmoja na Kibu

Aidha baada ya kukamilisha usajili wake, uongozi wa Simba ulipambana kuhakikisha Kibu anapata uraia wa Tanzania na hivyo kusajiliwa kama mchezaji wa ndani

Rais wa heshima klabu ya Simba Bilionea Mohamed Dewji ametaka Kibu aendelee kubaki Msimbazi hivyo baada ya mazungumzo hayo hatma yake itafahamika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.