Chelsea imezidisha juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk wa Ukraine mwenye thamani ya pauni milioni 65 Georgiy Sudakov, 21, ambaye pia anafuatiliwa na Arsenal, Manchester City na Liverpool.Mail)
Chelsea pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa zaidi ya £100m.(Sky Italia)
Kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak, 31, ni mchezaji mwingine ambaye yuko kwenye rada ya Chelsea msimu huu wa joto, huku klabu yake ya Uhispania ikitaka kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga upya kikosi.(Fichajes)
West Ham United na Tottenham Hotspur ndio walio mstari wa mbele kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, msimu huu wa joto, huku timu zote zikipanga kutoa takriban £50m.(Football Transfers) Mshambulizi wa Uswidi Viktor Gyokeres, 25, amekataa kutoa hakikisho la kusalia katika klabu ya Sporting Lisbon huku Arsenal kumtaka (Standard)
Manchester United inajaribu kutafuta mnunuzi wa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro mwenye umri wa miaka 32 msimu huu wa joto ili kujaribu kupunguza mzigo wao mishahara.(TEAMtalk)
Arne Slot, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja anayeondoka Jurgen Klopp huko Liverpool, anaweza kurejea Feyenoord ili kuwasajili kiungo wa kati wa Uholanzi Mats Wieffer, 24, na mlinzi wa Uholanzi Lutsharel Geertruida, 23.(Football Insider)
Sevilla ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia meneja wa Leicester City Enzo Maresca baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 kuiongoza timu hiyo kurejea Premier League.(Mail)
BBC



