Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imealikwa Saudi Arabia kushiriki michuano maalum ambapo itacheza mechi za Kimataifa za kirafiki dhidi ya Sudan
Mapema leo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliweka hadharani majina ya wachezaji katika kikosi kitakachosafiri Jumatano, May 08 2024
Kikosi hicho hakijamuisha nyota wa klabu za Yanga, Azam Fc na Simba ambazo zimewekeza nguvu katika mechi za kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya NBC
Hata hivyo Simba imemruhusu mlinda lango wake Ali Salim kujiunga na kikosi hicho




