Azam - Simba - Local

Azam Fc, Simba zachuana kuwania nafasi ya pili

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 May 2024
Azam Fc, Simba zachuana kuwania nafasi ya pili

Nyasi za Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam leo zitawaka moto katika mchezo wa kusaka heshima na nafasi ya kukata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

Azam FC leo wanakuwa nyumbani kuwakaribisha Simba, kwenye uwanja huo mchezo utakaochezwa saa 12:15 jioni huku timu zote zikihitaji matokeo katika mchezo huo

Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 53 ikiwa na mchezo mmoja mkononi huku wakiwa chini ya Azam kwa tofauti ya pointi nne huku Wanalambalamba hao wakishika nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga

Katika mchezo wa leo timu zote zinahitaji kupata matokeo chanya na endapo timu yoyote itaibuka na ushindi itajiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza nafasi ya pili na kuendelea kutoa msukumo kwa Yanga kwenye kuwania ubingwa msimu huu

Kama Simba ikipoteza mechi ya leo itajiweka kwenye nafasi ngumu ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya misimu zaidi ya mitano

Katika michezo 18 waliyokutana timu hizo, Simba imeshinda mara sita, imepoteza tatu na Azam FC imepata matokeo mara tatu na kupoteza sita, wote wametoka sare mara tisa

Kuelekea mchezo huo wa leo, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda alisema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wapo tayari kushindana kupata matokeo mazuri

Alisema wanatambua Azam ni timu nzuri yenye kutoa ushindani lakini wamejipanga kufanya vizuri na kuondoka na pointi tatu

"Siku zote mchezo wa mpira kuna makosa hayakwepeki, kikubwa ni kuyafanyia kazi katika uwanja wa mazoezi, mechi iliyopita tulifanya makosa naamini tumesahihisha na kuyapunguza tayari kwa mchezo wa leo"

"Soka ni mchezo wa wazi hakuna kuficha, tunaingia uwanjani kusaka pointi tatu ambazo ni muhimu sana, leo tutaendelea kumkosa Chama (Clatous) ambaye ni majeruhi na anatumikia adhabu, Miquison, Ntibazonkiza, Onana wote ni majeruhi pia, lakini hiyo sio tatizo kwa kuwa wachezaji waliopo ni waajiriwa wa Simba atakayepewa jezi atatakiwa kutumikia timu na kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Mgunda

Kocha wa Azam FC, Bruno Ferry alisema mara ya mwisho walikutana na Simba katika mashindano ya Muungano na kupoteza, hivyo wataingia uwanjani kwa tahadhari wakitaka pointi tatu

Alisema wamejipanga vizuri, wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na kusaka pointi tatu muhimu mbele ya wapinzani wao kwa ajili ya kufikia malengo yao

"Ni mechi ya ushindani mkubwa, Simba wako vizuri, tumefanya maandalizi mazuri na wachezaji wapo tayari kwa mchezo, naomba waamuzi kuwa waungwana kwa sababu maamuzi mengi yamekuwa yakiharibiwa, wawe makini ili uwe mchezo wa haki," alisema Bruno

IPP Media

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
23m ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
3h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
4h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
5h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
7h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’