Simba - Local

Simba yajipanga na vita ya nafasi ya pili

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 May 2024
Simba yajipanga na vita ya nafasi ya pili

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewapa pole Wanasimba wote baada ya jitihada za kuwania ubingwa ligi kuu msimu huu kufika tamati jana

Ahmed amesema licha ya machungu wanayopitia, hawapaswi kukata tamaa kwani mechi nne zilizobaki ni muhimu sana katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya pili

Ahmed amesema Simba lazima ijihakikishie tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao kwani kama wataikosa nafasi hiyo maumivu yatakuwa makali zaidi

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;

"Leo ni usiku mgumu kwetu uliojaa maumivu na uchungu mkali

Lakini hatuna budi kukubali kuwa huu ndio ushindani

Kitu muhimu wana Simba ni kutambua kuwa kwetu ligi haijaisha

Tungali bado mioyo yetu inavuja damu kwa uchungu wa kukosa taji lakini hatuna budi kusimama imara tuipiganie Simba yetu imalize nafasi ya pili

Hii ndio nafasi pekee yenye thamani tuliyobakiwa nayo kwa sasa, inawezekana usione uzito wa nafasi hiyo lakini tukiiikosa ndio utagundua tumepoteza kitu kikubwa kiasi gani

Lets go wana Simba kila vita ina hatua zake tumepoteza hatua ya kwanza sasa tupambane tushinde ya hatua pili

Tukifanikiwa kushinda vita ya hatua ya pili, turudi kambini tujipange kuanza upya kwa msimu ujao"

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’