Yanga - Local

Chopa kutumika Paredi ya ubingwa Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 May 2024
Chopa kutumika Paredi ya ubingwa Yanga

Jumamosi May 25 2024 mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga watakabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya NBC 2023/24 baada ya kufanikiwa kulitetea kwa msimu wa tatu mfululizo

Katika kufanya siku hiyo kuwa ya kipekee, NBC Bank wameandaa matukio ya aina yake jijini Dar es salaam

Akizungumza katika Mkutano wa pamoja na Wanahabari kati ya Yanga na NBC Bank, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Helkopta (chopa) maalum imeandaliwa kwa ajili ya kufanya paredi la ubingwa jijini Dar es salaam

"Kuanzia saa 5 asubuhi kutakuwa na Helkopta itakayofanya paredi ya ubingwaΒ  ndani ya Jiji la Dar es salaam"

"Hili litakuwa tukio la kwanza na la aina yake kufanyika hapa Afrika, sisi tunakwenda kuwafundisha namna ubingwa unasherehekewa"Β 

"Baada ya kufanya parade maeneo mbalimbali, saa 9 Alasiri Helkopta itatua uwanja wa Benjamin Mkapa kuleta kombe"

"Yaani wakati mashabiki wa Yanga wakiwa tayari wameujaza uwanja wa Mkapa, Helkopta itatua, kombe litakabidhiwa kisha itaondoka," alisema Kamwe

Yanga ni mabingwa tangu Bank ya NBC ilipoanza kudhamini ligi kuu ya Tanzania Bara. Likiwa taji la tatu ambalo Yanga watakabidhiwa kuwa mali yao

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’