Azam - Local - Transfer

Azam yashusha Straika kutoka Colombia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 May 2024
Azam yashusha Straika kutoka Colombia

Klabu ya Azam Fc imeendelea kufanya maboresho ya kikosi kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao ambapo timu hiyo imetangaza kumsajili mshambuliaji Jhonier Blanco raia wa Colombia

Azam Fc wamethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mapema leo;

"Tunayo furaha kutangaza kwamba tumekamilisha uhamisho wa mshambuliaji raia wa Colombia, Jhonier Blanco, kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya mji wa Rionegro, inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia.

Blanco aliyezaliwa Oktoba 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatuatia makubaliano baina ya klabu yake na Azam FC.

Alianzia soka lake kwenye akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas.

Akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya daraja la kwanza ya Fortaleza. Akiwa na klabu hiyo, akaibuka kuwa mfungaji bora akiisaidia kupanda daraja. Baada ya mkopo akarudi klabuni kwake Aguilas Doradas hadi sasa ambapo Azam FC imemnunua"

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’