Yanga - Local

Gamondi apania kutetea ubingwa FA

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 May 2024
Gamondi apania kutetea ubingwa FA

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kuwa na msimu mzuri bado wana kazi ngumu mbele yao katika fainali ya kombe la Shirikisho la CRBD Bank dhidi ya Azam Fc

Katika fainali hiyo Yanga atakuwa ugenini mbele ya wenyeji Azam Fc, mchezo utakaochezwa Juni 2, mwaka huu uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar, saa 2:15, usiku

Gamondi amesema anafurahi kufikia malengo yao kwa kutwaa taji la ligi pamoja na mchezaji wake Stephane Aziz Ki kufanikiwa kumaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji bora

"Mwanzoni mwa msimu niliwaambia kuhusu Aziz Ki, kuwa ni mchezaji mkubwa na atafanya mambo makubwa anachukuwa tuzo ya mfungaji bora ni jambo la kujivunia. Licha ya yote lakini bado hatujamaliza kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni fainali," amesema Gamondi

Amesema wana fainali ya Shirikisho dhidi ya Azam Fc, hautakuwa mchezo rahisi lakini anaimani na vijana wake watafanya vizuri na kufanikiwa kutwaa taji hilo ambalo wanalishikilia kwa misimu miwili mfululizo

"Msimu huu tumecheza vizuri, nimekuwa na timu bora, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji na tumefanikiwa kutoa mfungaji bora sasa tunataka kushinda taji la FA"

"Fainali ni kati ya timu mbili na mmoja apate ushindi. Yanga kwangu ni timu bora kwa hapa nchini na tunaenda kucheza fainali kwenye uwanja mzuri ambao unachezeka vizuri" 

Gamondi ameeleza kuwa haitakuwa fainali rahisi kulingana na mechi ya mwisho walipokutana na Azam Fc, walipoteza hali ambayo hataki kuona inajirudia katika fainali hiyo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
3h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’