Simba yasaka Mkurugenzi wa Mashabiki na Wanachama

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th June 2024


Simba yasaka Mkurugenzi wa Mashabiki na Wanachama

Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba imewatangazia Wanachama wake kuwa inakaribisha maombi ya kazi ya mkataba nafasi ya Mkurugenzi wa Mashabiki na wanachama

Akizungumza kuhusu nafasi hii Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema;

"Hii ni nafasi muhimu sana katika klabu yetu hivyo tunakaribisha waombaji wenye vigezo vilivyotajwa hapo juu kuleta maombi yao ndani ya muda uliopangwa"

"Tumedhamiria kuimarisha Idara ya Wanachama na Mashabiki ili kuwapa Wanachama wetu huduma bora, kusogea karibu yao na kuboresha uandikishaji wanachama baada ya Katiba ya Simba kuondoa ukomo wa namba ya Wanachama"


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.