Yanga - Local

SportPesa yakabidhi Mamilioni ya bonasi Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Jun 2024
SportPesa yakabidhi Mamilioni ya bonasi Yanga

Kampuni ya SportPesa ambao ni Wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga, leo wamekabidhi fedha za bonasi kwa klabu hiyo baada ya kufikia mafanikio yanayokidhi makubaliano ya kimkataba

Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu, kombe la Shirikisho la CRDB pamoja na kufika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika Masaki jijini Dar es saalam mapema leo, Mkurugenzi wa SportPesa Abbas Tarimba amewapongeza viongozi wa Yanga kwa kuongoza klabu hiyo kwa weledi ambao ni chachu ya mafanikio yao

SportPesa imeikabidhi Yanga hundi yenye thamani ya Tsh 537,500,000/- ambayo ni fedha za bonasi kutokana na mafanikio waliyopata msimu uliomalizika

"Yanga imekuwa ikiendeshwa kiuweledi. Hii inatokana na kuwa na Viongozi wenye njaa ya mafanikio. Nguvu hiyo imeifanya kuingia kwenye moja ya Klabu bora tatu barani Afrika"

"Nimpongeze sana Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa jitihada zake kwa Klabu hii. Sisi kama Kampuni ya SportPesa vile vile tunampongeza Mdhamini na Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa mchango wake mkubwa kwa Klabu hii. Bila shaka amefanya kazi kubwa, tunapenda salamu zetu zimfikie"

"Leo tunakabidhi mfano wa Hundi kwa Klabu ya Yanga kama BONUS ya mafanikio ya msimu. Hundi hii ina Thamani ya Tsh 537,500,000/= ambayo itawekwa kwenye akaunti za benki za Yanga"

"Nawashukuru pia Wachezaji na benchi wa Yanga kwa kile walichokifanya pale Zanzibar. Licha ya Wachezaji wetu wawili muhimu kukosa penati za mwanzo bado hawakupoteza malengo ya kuipambania nembo ya Klabu yetu" alisema Tarimba

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’