Klabu ya Azam Fc imetangaza kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Adam Adam
Adam anatua Azam Fc akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza kuitumikia klabu ya Mashujaa Fc ya mkoani Kigoma
"Baada ya kucheza miaka 10 nje ya viunga vya Azam Complex, hatimaye tumemrejesha kijana wetu, Adam Adam. Tunathibitisha kuwa tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja, tayari kabisa kuitumikia Azam FC msimu ujao 2023/24," taarifa ya Azam Fc ilibainisha



