Taarifa ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba upande wa Mwekezaji kujiuzulu zilianza kuvuja jana jioni, baada ya Rais wa Heshima klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji kuwataka wajiuzulu nafasi zao
Kujiuzulu kwa Wajumbe hao kunakwenda sambamba na kujiuzulu kwa Mtendaji Mkuu ambaye pia anapaswa kuachia nafasi yake ili kupisha mabadiliko hayo
Mmoja wa Wajumbe wa Bodi Rashid Shangazi amethibitisha kuachia nafasi yake kuitikia wito wa Mo ambaye ndiye aliyefanya uteuzi wake
"Mimi binafsi bila kuwazungumzia wenzangu ni kweli nimejiuzulu nafasi yangu kwenye bodi ,ikitokea mwekezaji ataona nafaa tena mbeleni basi naweza kurudi kumsaidia," alisema Shangazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah 'Try Again' nae inaelezwa tayari amejiuzulu ili kupisha safu hiyo mpya ya uongozi
CEO wa zamani Barbara Gonzalez anatajwa kurejeshwa na pengine kutakuwa na sura nyingine mpya zitashuhudiwa
Hata hivyo mabadiliko hayo yatahusisha upande wa Mwekezaji tu, upande wa Wanachama unaongozwa na Murtaza Mangungu hakuna aliyejiuzulu na wenye dhamana ya kuwajibisha ni Wanachama wenyewe