Klabu ya Yanga leo Jumapili, Juni 09 2024 inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama
Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 4 asubuhi katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere
Hizi hapa Ajenda za Mkutano huo;
- Kufungua Mkutano
- Kuhakiki Wajumbe waaliohudhuria Mkutano huo
- KUthibitisha Ajenda
- Kuthibitisha kumbukumbu za Mkutano uliopita
- Yatokanayo na kumbukumbu za Mkutano uliopita
- Hotuba ya Rais
- Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji
- Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya klabu
- Kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofuata
- Kufunga Mkutano



