Yanga - Local

Yanga yahakikishiwa eneo la kujenga uwanja

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Jun 2024
Yanga yahakikishiwa eneo la kujenga uwanja

Serikali imeiruhusu Yanga kujenga uwanja wake wa kisasa katika eneo la Jangwani yalipo makao makuu ya klabu, Jangwani jijini Dar es salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amebainisha hayo leo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Yanga

Mh Mchengelwa alisema kwamba Yanga imepewa muda maalum wa kukamilisha ujenzi huo wa uwanja na kwamba ikishindwa itanyang'anywa

"Tumewapa muda wa kuyafanyia kazi yale ambayo tumewaambia kwenye uwanja huo, ila mkishindwa tutawanyang'anya, tumewapa kipimo, hivyo mzingatie iendane na mpango wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu, kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa," alisema

Mbali na Yanga, alisema Tamisemi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Michezo na BMT, watachagua wachezaji bora ambao watakuwa wanakuza vipaji vya watoto

"Nimeambiwa Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Michezo nchini, Ally Mayay na Edibily Lunyamila ni zao la UMITASHUMTA na UMISETA, ndio maana chini ya Rais Samia anawekeza nguvu katika michezo mashuleni"

"Namshukuru rais wa Yanga, Injia Hersi Said kwa kuendesha klabu yenye mafanikio makubwa, ikiwemo uwekezaji na usajili wa wachezaji wazuri na kuleta utulivu wa Yanga, nakumbuka miaka kadhaa iliyopita kabla ya uongozi wa Injinia Hersi, tulifanya kazi kubwa na nilikuwa sehemu hiyo ya mabadiliko, utulivu huo umeleta mafanikio makubwa chini ya Injinia na sasa Yanga inafanya vizuri ligi ya ndani hadi kimataifa," alisema

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’