Simba - Local

Dewji ataka utulivu Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Jun 2024
Dewji ataka utulivu Simba

Mfadhili wa zamani wa klabu ya Simba Azim Dewji amewataka Wanachama na Mashabiki kuwa watulivu na kutumia njia za kistaarabu kutatua changamoto zilizopo

Azim amesema haungi mkono shinikizo la mashabiki kwa baadhi ya viongozi kuwataka wajiuzulu kwani njia hiyo haiwezi kuwasaidia

"Mimi naamini Simba tulikuwa na timu nzuri msimu uliomalizika. Tumekosa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao tu lakini tumefunga pointi na Azam Fc hivyo naweza kusema na sisi ni wa pili"

"Lazima tukubali ushindani ulikuwa mkubwa, washindani wetu nao walikuwa wamejipanga, hatukuwa na timu mbaya"

"Tutumie njia za kistaarabu kutatua changamoto zilizopo, tusichukue maamuzi ya kukurupuka kwani tunaweza kuharibu," alisema Dewji

Aidha Dewji amewashauri viongozi wa Simba kujitokeza hadharani haraka kuwatuliza mashabiki huku akiwataka pia kuhakikisha wanasimamia vizuri usajili wa dirisha kubwa sambamba na kutafuta kocha ambaye atakaa kwa muda mrefu badala ya kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiiathiri timu

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’