Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amethibitisha kujiuzulu nafasi yake
Akizungumza katika mahojiano maalum na Azam TV, Try Again amesema baada ya majadiliano na Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' ambaye pia ni Rais wa heshima wa Simba, amesema ameondoka katika nafasi yake ili kumpisha Mo Dewji kurudi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi
"Tumefanya majadiliano ya kina na Mwekezaji wetu (Mo), nimemshauri kwa maslahi mapana ya klabu anapaswa kurudi kuongoza Bodi ya Wakurugenzi"
"Maneno yamekuwa mengi, kutoka kila upande ukweli ni kwamba tumewaumiza mashabiki wetu na naamini huu ni wakati wa kuirudisha nguvu ya Simba"
"Tunawaomba mashabiki na wajumbe wa Bodi tuache marumbano, tuonyeshe uimara wetu kama slogan yetu inavyosema, SIMBA NGUVU MOJA," alisema Try Again
Ni rasmi sasa Mo anarejea kuongoza Bodi na bila shaka atakuwa na nafasi nzuri ya kusimamia kila mkakati wa klabu kuanzia usajili