Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Juni 22 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jun 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Juni 22 2024

Manchester United wamefanya mawasiliano ya awali na Lille kuhusu usajili wa beki wa Ufaransa Leny Yoro, 18. (Sky Sports)

Wolves wanataka hadi £45m kwa Max Kilman kufuatia ofa ya West Ham ya £25m kwa mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27. (Guardian)

Manchester United na Tottenham wanamtaka Jonathan David wa Lille, Wolves wakitaka pauni milioni 45 kwa ajili ya Max Kilman, huku Douglas Luiz anakaribia kuondoka Aston Vila

Manchester United na Tottenham ni vilabu viwili kati ya vilabu vinavyomhitaji mchezaji wa Canada mwenye umri wa miaka 24 na mshambuliaji wa Lille Jonathan David. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, anakaribia kuhama kutoka Aston Villa kwenda Juventus , huku Villa ikipokea winga Mwingereza Samuel Illing-Junior, 20, na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Barrenechea, 23, pamoja na ada ya uhamisho ya £25m. (Mail)

Lazio wako tayari kumpa mlinda lango wa Ugiriki Christos Mandas, 22, pamoja na ada ya pauni milioni 15 katika jitihada zao za kumsajili mshambuliaji Muingereza Mason Greenwood, 22, kutoka Manchester United . (Il Messaggero - in Italian)

Southampton wanapanga kumnunua winga wa Jamaica na Fulham Bobby De Cordova-Reid, 31, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto. (JSun)

Beki wa Manchester United na England Aaron Wan-Bissaka, 26, anakaribia kuhamia Galatasaray na atapewa mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya Uturuki. (Bein Sports Turkey - in Turkish)

Chelsea na Bayern Munich zote zinaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Mhispania Marc Guiu, 18 , ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 6m (£5.08m). (Fabrizio Romano)

West Ham na Nottingham Forest wamewasiliana na Arsenal kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Uingereza Reiss Nelson, 24 (Football Insider)

Manchester United wana wasiwasi kwamba hawataweza kumnasa Rennes mwenye umri wa miaka 19, Desire Doue kwenda Old Trafford, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikiweka bei ya juu inayomtaka kiungo huyo. (Givemesport) ya nje

West Ham na Brentford wameonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27. (FootballTransfers)

Roma wako tayari kufanya mazungumzo na Manchester City huku wakitafuta njia za kumnunua mlinzi wa Uhispania Sergio Gomez, 23. (Caughtoffside)

AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28. (Corriere dello Sport via Football Italia), ya nje

Everton wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Senegal Illian Ndiaye, 24, kutoka Marseille . (L'Equipe - in French) Bayern Munich wako kwenye mazungumzo na Paris St-Germain kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 21. (Sky Sports Germany)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’