Mkoa wa Morogoro siku ya leo Jumamos utapata ugeni mkubwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ambapo Wananchi watafurika kushuhudia Tamasha la Wape Tabasamu lililoandaliwa na nyota wa Yanga Kibwana Shomari na Dickson Job
Ni mechi ya 'charity' kwa ajili ya kuchangisha fedha ambazo zitakwenda kusaidia wale wenye changamoto mbalimbali
Ni msimu wa tatu Job na Kibwana wanaandaa Tamasha hili lakini mwaka huu linaonekana kuwa na mvuto zaidi
Ushindani ni mkali kuanzia katika usajili wa wachezaji lakini hata 'mabosi' nao kuchagua upande
GSM pamoja na Arafat Haji wao wamechagua upande wa Kibwana wakati Injinia Hersi Said yeye yuko upande wa Job
Wachezaji kama Pacome Zouzoua, Clatous Chama, Prince Dube wanatarajiwa kuitumikia timu Job wakati vinara wa mabao ligi kuu msimu uliopita Stephane Aziz Ki aliyekuwa mfungaji bora na Feisal Salum aliyeshika nafasi ya pili wako timu Kibwana bila kumsahau Mukoko Tonombe
Kumekuwa na matukio ya 'kuporana' wachezaji ambapo beki Ibrahim Bacca ambaye awali alitangaza kuwa timu Kibwana jana alionekana akisaini kuitumikia timu Job kwa kile alichoeleza timu Kibwana hawana hela!
Ni katika 'kunogesha' Tamasha hilo ambalo mafanikio yake yatapeleka Tabasamu kwa watu wengi zaidi
Kutakuwa na treni ya mwendokasi kutoka jijini Dar es salaam ambayo itapeleka mashabiki mkoani Morogoro na kuwarudisha Dar baada ya mchezo
Azam TV nao watakuwa mbashara Baraka Mpenja akipewa jukumu la kuhabarisha yatakayojiri dimba la Jamhuri kuanzia saa 10 jioni