Simba yavuna Mamilioni baada ya kumuuza Inonga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Jun 2024
Simba yavuna Mamilioni baada ya kumuuza Inonga

Jana klabu ya Simba ilithibitisha kumuuza beki Hennock Inonga Baka kwenda klabu ya FAR Rabat inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco

FAR Rabat wamelazimika kununua mkataba wa mwaka mmoja ambao Inonga alikuwa amebakisha na Simba baada ya jaribio la beki huyo kutaka kuvunja mkataba wake 'kienyeji' kukwama

Kupitia dili hilo, Simba inatajwa kuvuna takribani Tsh Milioni 500, fedha ambazo pasipo na shaka zitatosha kushusha beki mwingine wa daraja la juu kuchukua nafasi yake

Tayari Simba ilishaanza mapema msako wa kutafuta beki mpya wa kati ikiendelea na mazungumzo na mabeki wa maana kuungana na Lameck Lawi ambaye tayari Simba imemsajili kutoka Coastal Union

Inonga ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri katika michuano ya Afcon iliyopita akiwa na kikosi cha DR Congo, jambo lililosababisha timu mbalimbali kutamani huduma yake msimu ujao.

Akiwa Simba, Inonga ambaye alijiunga na timu hiyo Agosti 2021 amekuwa mchezaji muhimu katika eneo la beki wa kati akiingia kikosi cha kwanza moja kwa moja huku akifanikiwa kufunga mabao matano ndani ya Ligi Kuu.

Beki huyo anakumbukwa na wana Simba alipofunga bao kwa kichwa dakika ya pili dhidi ya Yanga pale Wekundu hao waliposhinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 16, 2023.

Mbali na kufanya mazuri ndani ya Simba ikiwemo kuisaidia kushinda Ngao ya Jamii msimu uliopita (2023-2024), lakini dakika za mwisho mwisho mwa msimu uliopita Inonga hakuwa na maelewano mazuri na uongozi wa klabu hiyo baada ya kuingia kwenye mgogoro wa kimkataba ambapo mwenyewe alidai unamalizika Juni 30, 2024 ilhali Simba wakisema utamalizika Juni 30, 2025.

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
3h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
5h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
5h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
6h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
7h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
10h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
12h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
13h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
13h ago
READ MORE β†’